Mwanafunzi wa kidato cha 3 Kisii aaga dunia baada ya kupigwa na kiranja

Hali ya majonzi imeikumba Shule ya Upili ya St Joseph Nyabigena iliyopo Gucha Kusini, Kaunti ya Kisii hii ni kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao anayedaiwa kupigwa na kiranja. Mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu anadaiwa kuaga dunia baada ya kukimbizwa katika Hospitali ya Wamishonari ya Tabaka.

Kulingana na ripoti ya Nation, marehemu alianguka na kuzimia baada ya kupigwa na kiranja, na inadaiwa walizozana kabla ya kisa hicho cha asubuhi ya Jumanne 26.

“Marehemu alikuwa akisoma Bibilia kuelekea 7am. Baada ya mgogoro kidogo kati yao kiranja alimpiga kofi kisha teke la tumbo na hapo alianguka na kuzimia,” mmoja wa wanafunzi alisema. Usimamizi wa hospitali ulikataa kusema na wanahabari kuhusu kilichosababisha kifo cha mwanafunzi huyo.

https://kiswahili.tuko.co.ke/299376-mwanafunzi-wa-kidato-cha-3-kisii-aaga-dunia-baada-ya-kupigwa-na-kiranja.html#299376

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s